Mmarekani mwenye asili ya kisomali amesema mtoto wake wa kiume
ametoroka marekani kwenda kujiunga na kundi la kiislamu lenye msimamo
mkali nchini Syria.
Katika mahojiano maalumu na idhaa ya kisomali ya Sauti ya Amerika
baba wa kijana huyo mwenye umri wa miaka 19 Mohamud Mohamed amesema
mtoto wake wa kiume aliondoka katika mji wa Minneapolis Julai 18 na
akampigia mama yake simu akiwa Syria siku nne baadae na kumwambia
alikuwa na ‘ kaka zake”.
Baba wa kijana huyo amesema Mohamed ambaye kwa kawaida anaishi na
mama yake nchini Canada alikwenda Minneapolis kukaa naye kwa muda
wakati wa kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani. Amesema Mohamed
alitoweka bila tahadhari akisema alikuwa anaenda msikitini kwa ajili ya
sala za Ijumaa.
Amesema ilikuwa mshtuko. Mtoto wake alikuwa mwanafunzi alibadilika
ghafla. Alikuwa anasali lakini aliongeza kusali masaa 24 na mara chache
sana alikuwa mbali na misikiti. Alipanga safari yake bila baba yake
kujua na akaishia Syria. Anasema wote katika familia wameshtushwa sana,
hawakutegemea angeweza kufanya hivyo.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 19 alikwenda Uturuki njia ambayo
inatumiwa na watu wa nchi za magharibi wanaotaka kujiunga na Islamic
State na makundi mengine ya wanamgambo yanayofanya operesheni zake
nchini Syria.
Hadithi yake ni sawa na ya wasomali wengine waliondoka marekani
wakitaka kwenda kupigana sambamba na makundi kama hayo. Wasomali wawili
kutoka jimbo la Minesota Abdiraham Muhumed na Douglas MacArthur McCain
wameuwawa katika mapigano nchini Syria
No comments:
Post a Comment