Home Traders

Home Traders

Tembelea TK FM Redio 88.5 Tanga

Friday, 7 November 2014

Aly Ame Zungu hauzwi Simba wala Yanga-Kifaru

Akizungumza kwa majigambo kama ilivyo kawaida yake msemaji wa  Mtibwa  Thobias Kifaru amesema kua hafikirii kwa mchezaji wao nguli na mpachika nyavu tishio msimu huu Tanzania Aly Ame Zungu  kama atauzwa kwenda   simba wala Yanga.
Meck Mexime

Akizungumza na TK Kifaru amekanusha uvumi uliozagaa hapa nchini kua mshambuliaji huyo anaweza kuondoka katika timu hiyo ya wakata miwa wa mtibwa sugar.
Kifaru aliendelea kusema kua nguli huyo hawezi kufanya hivyo kutokana na kuhofia kama waliyowakuta baadhi ya wachezaji wa timu hiyo ambao walikua tishio na kuihama timu hiyo na matokeo yake wamekaa benchi na kupoteza viwango vyao.
Akimalizia kuitanabaisha TK Kifaru alisema kuwa labda mchezaji huyo auzwe nje ya nchi lakini si hapa tanzania kwa timu za Simba wala yanga.

No comments:

Post a Comment