Wagosi wa kaya Coastal union imelia na mwamuzi wa mchezo wake dhidi ya Azam fc uliopigwa leo hii pale chamanzi na kupokea kichapo cha mabao mawili kwa moja.
Kwa mujibu wa msemaji wa Coastal union Oscer Asenga amesema kuwa mwamuzi wa mchezo huo wa leo kuongeza kwake dakika ndiko kulipoifanya timu hiyo kufungwa bao la pili dakika hizo za mwisho kabisa kufuatia kumalizika kwa dakika nne za mwisho zilizokua zimeongezwa.
Bado historia inawahukumu wagosi hao wa kaya coastal katika uwanja wa chamanzi kwani imekua ikifungwa na Azam katika dimba hilo.
Akizungumza na Tanga Kunani TK Asenga amendelea kusema kuwa kilichotokea ndicho hicho na kimewafanya kuwanyiwa ushindi timu hiyo.
Licha ya kupoteza mchezo huo washabiki wa timu hiyo wasikate tamaa na timu itajipanga kwa ajili ya mchezo unaofata.
No comments:
Post a Comment