Mchezaji bora wa VPL kwa mwezi Oktoba, Salum Abubakar wa
Azam atakabidhiwa zawadi yake kesho (Novemba 8 mwaka huu) kabla ya mechi
kati ya Azam na Coastal Union.
Abubakar ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa
Stars) aliwashinda wachezaji wengine 20, huku wanne kati ya hao
wakichuana naye kwa karibu.
Wachezaji hao ni Joseph Mahundi wa Coastal Union, Salim Mbonde
(Mtibwa Sugar), Rashid Mandawa (Kagera Sugar) na Najim Magulu wa JKT
Ruvu Stars.
Kwa kuibuka mchezaji bora, Abubakar atazawadiwa kikombe na fedha
taslimu sh. milioni moja kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya
simu za mkononi ya Vodacom.
Jopo maalumu la makocha waliopo katika viwanja vyote vinavyotumika
kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ndiyo wanaofanya kazi ya kuchagua
mchezaji bora kwa kila mechi kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa, na
baadaye alama zao kujumlishwa ili kumpata mshindi wa mwezi.
No comments:
Post a Comment