Young Africans imebuka na ushindi wa
mabao 2-0 dhidi ya timu ya JKT Mgambo ya jijini Tanga mchezo uliofanyika
jioni ya leokatika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku Saimon
Msuva akibuka shujaa kwa kukwamisha wavuni mabao yote mawili.
Young Africans iliuanza mchezo kwa kasi kwa lengo la kusaka mabao ya
mapema, lakini kutokua makini kwa washambuliaji wake Jaja, Coutinho na
Ngasa kulipelekea kukosa mabao ya wazi dakika 45 za kipindi cha kwanza
na kufanya timu kwenda mapumziko zikiwa 0-0.
Kipindi cha pili
Young African illifanya mabadiliko kwa kuwatoa Haruna Niyonzima na
Geilson Santos "Jaja" na nafasi kuchukuliwa na Saimob Msuva na Jerson
Tegete ambao waliongeza kasi ya mchezo na mashambulizi langoni mwa
Mgambo JKT.
Dakika ya 74 ya mchezo, Saimo Msuva aliipatia Young
Africans bao la kwanza baada ya kuitendea vyema pasi ndefu ya kiungo
Mbuyu Twite aliyompenyezea na kumkuta mfungaji ambaye aliudokoa mpira
huo na kujaa wavuni na kumuacha mlinda mlango wa Mgambo JKT Said Lubawa
akigaa bila ya kujua cha kufanya.
Baada ya bao Mgambo JKT
walicharuka na kufanya mashambulizi kadhaa langoni kwa Young Africans
kwa lengo la kusaka bao la kusawazisha, lakini mashambulizi yao yalikuta
yakiokolewa na na walinzi wa Young Africans pamoja na mlianda mlango
Deo Munish "Dida"
Huku baadhi ya washabiki wakianza kutoka nje
wakijua mchezo umemalizika kwa ushindi wa bao 1, Saimon Msuva tena
aliipatia timu yake ya Young Africans bao la pili baada ya pasi
aliyotanguliziwa na kiungo Hassan Dilunga kuitumia vyema na kuachikia
shuti lililojaa wavuni moja kwa moja.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizka, Young Africans 2 - 0 Mgambo JKT.
Kwa
ushindi wa leo Young Africans inakamata nafasi ya tatu nyuma ya Azam
FC iliyoko nafasi ya pili huku wakiwa sawa kwa kwa point na mabao ya
kufunga na kufungwa, Mtibwa Sugar wakiendelea kushika nafasi ya kwanza.
No comments:
Post a Comment