Home Traders

Home Traders

Tembelea TK FM Redio 88.5 Tanga

Thursday, 9 July 2015

Baraza la Madiwani Halmashauri ya Muheza Lavunjwa Rasmi,Mheshimiwa Kiroboto sasa kuachana na Siasa a uongozi

Baraza la halmashauri ya muheza jana limevunjwa rasmi na mwenyekiti wa baraza hilo Mheshimiwa Amiri  Kiroboto huku
akiidhinisha mafanikio yaliyopatika katika kipindi kizima cha miaka mitano yake lakini pia akizitaja changamoto kubwa zilizokuwa zikiikabili halmashauri ya Muheza. 
Mwenyekiti wa Halamashauri ya Muheza Amiri Kiroboto Kushoto (Picha Maktaba)


Akizungumza katika kipindi cha AMKA NA TK  kinachorushwa na kituo cha 88.5 TK FM  Mheshimiwa Kiroboto amesema kuwa baraza hilo limevunjwa kwa mujibu wa maelekezo  toka TAMISEMI kwa madiwani na mabaraza yao yote yavunjwe siku hiyo.


Kiroboto amesema kuwa changamoto  nyingi sana amekutana nazo kutokana na kuwa na madiwani takribani  46 huku kila mtu akiwa na fikra zake lakini kikubwa walikabiliana nazo kwani tangu waanze mwaka 2010 hadi sasa wapo salama na hakuna hata ugomvi uliojitokeza katika baraza lake wala mgomo.


Lakni changamoto kubwa amezitaja kuwa ni katika miradi ya maendeleo huku asilimia kubwa ikifikiwa katika suala zima la utekelezaji wa Maji.
 Wakati huo huo  Kiroboto amesema kuwa hayupo tayari tena kugombea katika  nafasi yoyote ile ya juu ya Uongozi na sasa inatosha ilobaki ni kuwachia wengine ili waweze  kuongoza.

Mheshimiwa Kiroboto amewashukuru sana wakazi wa muheza na kuwaacha na neno la kuondokea kwa kuwaambia kuwa anawapenda sana wana Muheza  "Muheza ni Kwangu na wana Muheza ni wangu" akamaliza kusema kuwa kuwa  huwezi kuitwa jemedari  kama hukuishinda mitihani hivyo anashukuru anaondoka madarakani  akiiacha Muheza ikiwa salama.

No comments:

Post a Comment