Watanzania wametakiwa kuhakisha kuwa
katika kipindi hiki ambacho taifa linafanya uchaguzi mkuu wanahakikisha
kuwa hawawachagui viongozi ambao wana aina yoyote ya doa la rushwa na
wenye uchu wa madaraka kwani kwa kufanya hivyo kuna uwezekano mkubwa wa
nchi kuingia katika machafuko makubwa kwani watu hao watakapoingia
madarakani wataendesha nchi kwa manufaa ya kikundi kidogo cha mafisadi
ambacho kitakuwa kikiwazunguka.
Hayo yamesemwa na washiriki wa mdahalo maalum lililoandaliwa na
taasisi ya Mwalimu Nyerere lenye maudhuhi ya amani na umoja hasa katika
kipindi hiki ambacho taifa linaelekea katika uchaguzi mkuu huku
mkurugenzi wa taasisi iliyoanda kongamano hilo mzee Joseph Butiku
akisema katika mchakato unaoendelea sasa katika chama cha mapinduzi na
taifa kwa ujumla yapo mengi yameanza kufanyika kinyume na utaratibu.
Naye aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba mzee
Josesph Warioba amesema ni lazim taifa lirudi katika hadhia yake ya
awali na siyo kila mtu kijifanyia ambo kama anavyotaka kama vile hakuna
utawala wa sheria.
Profesa Mwesigwa Baregu katika mdahalo huo amesema nchi inaingia
katika uchaguzi ikiwa inaombwe la katiba jambo ambalo kama nchi
haitakuwa makini yatatokea mambo kama yaliyotokea huko Kenya ambapo watu
walpoteza maisha kwani nao walikuwa kwenye uchahuzi kama ilivyo
Tanzania kwa sasa.
Jaji mstaafuAamiri Manento na amabye alikuwa mwenyekiti wa tume ya
haki za binadamu akitoa mada amesema matatizo mengi yanaletwa na
serikali tena kupitia vyombo vyake vya dola kama polisi na hivyo
inapaswa kujiangalia upya .
Katika hatua nyingine mwanaharakaati na aliyewahi kuwa mjumbe wa
tume ya mabadilko ya katiba bw haumprey polepole ameutaka ukawa kuacha
ubinafsi na huku ccm akitaka kuhakisha katika mkutano wao unaeendelea
dodoma kuhakisha wanatoa jina la mtu safi ili kulinusuru taifa huku rais
chama cha wanasheria wa zanzibar akisema sheria zipo ili zilete
haki na siyo kukandamiza haki za watu.
No comments:
Post a Comment