Tani zaidi ya Elfu 20 za shehena ya mafuta aina ya Petrol na Diesel
zimeshushwa katika bandari ya Tanga tayari kuanza kusambazwa kwa
wafanyabishara mbalimbali nchini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo
la serikali la kutumia bohari kuu ya mafuta iliyopo jijini Tanga kwa
ajili ya kupunguza msongamano uliopo jijini Dar es Salaam.
Walizungumz na waandishi w habari hapo jana mara baada ya
meli ya mafuta ya kampuni ya
''Ardmore Sea Marine'' kuanza zoezi la kushusha
shehena ya mafuta, mkurugenzi mkuu wa huduma za nishati na madini nchini
Bwana Felix Ngamilagos amesema kuwa mwanzon wa mwaka huu timu ya wataalamu ianze kazi kwa ajili ya kuanza kutumika kwa bandari ya Tanga kuanza kazi mara moja.
Hata hivyo amesema kuwa mpango huo ni mkakati wa serikali wa
kuhakikisha kuwa foleni za magari makubwa kutoka mikoa mbalimbali
zinapungua ambazo pia zitasaidia kupunguza uharibifu wa mazingira na
miundo mbinu ya barabara.
Awali Katika kikao cha pamoja kilichoshirikisha wafanyabiashara wa
magari, viongozi wa dini, na kijamii, baadhi ya wajumbe wa kikao hicho
wameiomba serikali kutilia mkazo zoezi la ushushaji wa mafuta kwa ajili
ya uchumi wa serikali na wananchi wake kwa sababu kulikuwa hakuna sababu
ya serikali kuacha kutumia bandari ya Tanga yenye miundo mbinu ya
kutosha kupitishia shehena zake ambazo ndio nguzo kuu za kukuza uchumi
nchini.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Tanga akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mheshimiwa Said Magalula ametoa mchanganuo kuhusu tani elfu 2o za Mafuta hayo.
Kufuatia hatua hiyo muwakilishi wa mafuta inginia Michael Mjinja ametoa ufafanuzi kuhusu wakazi wa Tanga na fursa hiyo huku reli ya Tanga ikichukua nafasi yake na kurudi kama ilivyo awali huku wafanyabishara na
wananchi kwa ujumla kuchangamnkia fursa hiyo katika zoezi la kukuza
uchumi wao ili mkoa wa Tanga uweze kukuza pato la taifa na mtu mmoja
mmoja.
No comments:
Post a Comment