Home Traders

Home Traders

Tembelea TK FM Redio 88.5 Tanga

Thursday, 16 July 2015

Mchakato Wagombea CUF Tanga Waiva

Mchakato wa kuwapata wale watakopeperusha bendera ya
chama cha wananchi CUF  hatimae umekamilika kwa asilimia kubwa huku kata takribani tano zikisalia lakini zikiwa zipo katika hatua ya mwisho ambazo kata hizo  ni Magaoni,central,nguvumali,maweni na masiwani shamba

 Akizungumza na AMKA NA TK Diwani wa kata ya Mwanzange CUF Mheshimia Rashid Jumbe  amesema kuwa takribani wagombea wengi waliopitishwa ni wale wale isipokuwa kata ya Marungu ambae aliyekuwa Diwani wa kata hiyo Mheshiwa Mohamed Mambeya  amejiunga na chama cha Mapinduzi  CCM huku kata ya Tongoni aliyekuwa Diwani wa kata hiyo akishindwa katika kura za maoni. 
Diwani wa Kata ya Mwanzange Mheshimiwa Rashid Jumbe
  Akizitaja Kata ambazo tayari zimepata wagombea wake ni kata ya ngamiani Kaskazini-Mheshimiwa Akida,Kata ya Ngamiani Kati-Habibu Nabahani Mpa,Kata ya ngamiani Kusini-Musa Bakari Mbaruku,Kata ya Mwanzange-Rashid Jumbe,Kata ya Marungu-Mheshimiwa Bori,Kata ya Tongoni-Nasoro Mohamed,Kata ya Kirare-Mheshimiwa Mnangwa,Kata ya Tangasisi-Mohamed Haniu Pen,Kata ya Kiomoni-Mheshimiwa Mwakuro Bakari,Kata ya Mabawa-Mheshimiwa Mwasabu,Kata ya Chongoleani-Mheshimiwa Akida Mswahili Njama,Kata ya Mzizima-Kijana Muft,Kata ya Mabokweni-Jumaa Mbega,Kata ya Makorora-Omari Salehe Mzee.

  

Mheshimiwa Jumbe akizungumzia kuhusu suala zima la UKAWA kuachiana nafasi za ugombea katika  nafasi mbali mbali kutokana na nafasi zote za hapa Tanga kuonekana kama CUF wamezishikilia sana,amesema kuwa  UKAWA ipo  ila kwa sasa wanasubiri katika nafasi ile ya kumpata mgombea wa Urais   ikamilike ili wakae katika meza moja wafanye mazungumzo lakini watakaa kwa vigezo na nguvu ya chama itatumika kutokana na sehemu husika ili kupata maridhiano.



Mheshimiwa Rashid Jumbe amelitolea pia ufafanuzi kuhusu suala zima la ongezeko la majimbo kwa upande wake amesema kuwa   hakubaliani nalo labda jimbo la Handeni   anakubaliana nalo lakini hayupo tayari kuunga mkono ongezeko la majimbo ya uchaguzi   kwani kufanya hivyo ni kutumia viabaya pesa za umma.

No comments:

Post a Comment