Home Traders

Home Traders

Tembelea TK FM Redio 88.5 Tanga

Thursday, 16 July 2015

Mohamed Haniu Arudi kwa Kishindo Tangasisi

Aliyekuwa Diwani wa kata ya Tngasisi miaka ya 2015 na katibu
wa wilaya wa Chama cha wananchi CUF Mohamed Haniu hatimae amereja tena kuwania kinyanganyiro cha udiwani katika kata ya Tangasisi baada ya kukaa kando katika nafasi hiyo katika uchaguzi uliopita.


Akizungumza na AMKA NA TK KIPINDI kipindi kinachorushwa na TK FM REDIO Haniu amesema kuwa kilichomfanya arejee tena kuwania udiwani katika kata hiyo ni msukumo mkubwa wa wananchi katika kata hiyo kumuomba arejee tene kutokana na kudumaa kwa maendelea katika kata hiyo. 
 

Akizungumzia kuhusu siasa za Tanga  tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mkoa wa Tanga umekuwa CUF ina nguvu sana lakini imekuwa haitoi hata nafasi ya ubunge,Mheshimiwa Haniu amesema kuwa anaamini kuwa chama kinakwenda kwa awamu kwani walianza na nafasi nne wakati wanaanza na sasa wanapoelekea ni kukamata Halmashauri ya Tanga.


No comments:

Post a Comment