mgombea wa nafasi ya urais ndani ya CCM, mgawanyiko ndani
ya chama hicho umeeanza baada ya uwepo la wimbi kubwa la wanachama kuanza
kukihama huku zaidi ya vijana 50 wakijiunga na chama cha Demokrasia na
maendeleo Chadema.
Sasa ni rasm, Bw Maiko Litanda
aliyekuwa kiongozi wa kundi la M4U, lililokuwa likimuunga mkono mbunge wa
Monduli Edward Lowasa anasema maamuzi yaliyofanywa kwa manufaa ya wachache
ndani ya CCM kwa kumkata jina Bw Edward Lowasa wanasema hawakati tamaa na kwamba
safari yao ya matumaini bado inaendelea na sasa inahamia chama cha Democrasia
na maendeleo Chadema.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa M4U
anasema zaidi ya vijana 100 wamekwisha kujiunga na Chadema ambapo takribani kadi 50 pekee za vijana hao zimerejeshwa huku uongozi wa Chadema mkoa
ukiwahakikisha kuwafikisha salama katika safari ya matumaini.
Katika hatua nyingine chama cha ACT
wazalendo kimepokea wanachama 7 kutoka vyama vya upinzani ambapo wanadai
kuondoka kwao kunatokana na viongozi wa vyama hivyo kuwa na ombwe la uongozi
huku vingine vikiendeshwa kwa ukanda.
Vugu vugu hili linakuja siku kadhaa
zikiwa zimesalia kabla ya Ukawa kumuweka wazi mgombea wao wa urais huku kukiwa
na eti eti huenda mmoja wa vigogo wa CCM yuko mbioni kujiunga na umoja huo.
CHANZO ITV
No comments:
Post a Comment