Friday, 17 July 2015
NIGERIA:WATU 9 WAMEUAWA NA SHAMBULIO LA BOMU WAKATI WAKISHEREHEKEA SIKUKUU.Na RAMADHANI MAKERO
Jeshi la nchini Nigeri limesema kuwa takribani watu 9 wameuawa kwenye mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga kwenye mji wa kaskazini mashariki mwa nchi ya Damturu
Wanasema kuwa washambuliaji wote walikuwa ni wanawake,mmoja mwenye umri mkubwa na mwengine ni mtoto wa miaka kumi
Ripoti zingine zinasema kuwa idadi ya waliokufa ni kubwa
Mashambulizi mengine yalifanyika kwenye maombi ya kusheherekea sikukuu ya Eid Fitr ya kumaliza mwezi wa ramadhan
Mashambulizi kama hayo hulalamikiwa kwa kundi la kiislamu la Boko Haram ambalo limeongeza mashambulizi yake baada ya kuingia madarakakani kwa Rais Muhammadu Buhar wa nchi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment