Baraza la Mitihani nchini Necta leo
limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha sita na kusema kuwa
umefaulu umeongezeka kwa asilimia 0.61.
Akitangaza matokeo hayo mjini Zanzibar leo, Katibu
Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde alisema mwaka huu idadi ya ufaulu
ni asilimia 98.87 ikilinganishwa na asilimia 98.26.
Dk Msonde alisema jumla ya watahiniwa 38,853
wamefaulu mitihani hiyo kati ya watahiniwa 40,753 waliofanya mitihani
hiyo ya kumaliza kidato cha sita. Aliongeza kuwa kuna watahiniwa 35
ambao walishindwa kufanya mitihani yao baada ya kuugua ghafla. Dk Msonde
aliongeza kuwa kati ya waliofaulu, wasichana ni 11,734 na wavulana ni
27,119.
ANGALIA MATOKEO KIDATO CHA SITA HAPA
ANGALIA MATOKEO KIDATO CHA SITA HAPA
No comments:
Post a Comment