Umoja wa Katiba Ya Wananchi UKAWA unajipanga kikamilifu kumtangaza
mgombea wake wa kiti chaUrais kwa shamra shamra mgombea huyo ambaye
Watanzania wengi wanamsubiri kwa hamu kubwa, akizungumza mbele ya
waandishi wa habari katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es salaam hapo jana Jumanne 14 Julai 2015, Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR Mageuzi Mhe. James
Mbatia, amesema ndani ya siku saba watakuwa tayari wameshamtangaza mgombea wao.
Mbatia amesema kuwa wameafikiana na vyama vyote vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA , kila mmoja kwenye chama chake kwa kufuata demokrasia amechaguliwa mgombea mmoja na kwa mardhiano ya hali ya tumepata mgombea mmoja ambae tunajipanga kumtangaza kwa mashamsham” alisema Mhe. Mbatia.
Swala lingine alilolizungumzia Mhe. Mbatia ni la uvumi ya kwamba CUF
imejitoa UKAWA, akijibu swali hilo lililoulizwa na mwandishi wa habari,
Mhe. Mbatia alisema kwamba taarifa hizo hazina ukweli wowote kwani
ameongea na Profesa Lipumba na kauli yake ya mwisho amesema yeye yupo
UKAWA, kwa hiyo taarifa zilizoenea kwamba CUF imejitoa UKAWA sio za
kweli, ila Mhe. Lipumba alikuwa na majukumu ya kikazi ndo maana hakuwepo
kwenye kikao hicho.
Kuhusiana na Mhe. Lowassa kuhamia UKAWA kama taarifa zilivyotapakaa
kwenye mitandao, Mhe. Mbatia amesema huo ni uzushi tu, kwenye mitandao
kila mmoja anaandika lake, mbona baada ya Mhe. Edward Lowassa kukatwa
kugombea kiti cha Urais kupitia CCM habari zilienea kwenye mitandao kuwa
amehamia ACT Wazalendo lakini taarifa hiyo haikuwa na ukweli wowote ni
taarifa za mitandaoni tu.
Mhe. Mbatia akuzungumzia kwanini kikao kimekuwa kirefu hivyo,
alisema licha ya kuwa na mchakato mrefu wa kumpata mgombea wa Urais
kupitia UKAWA katika uchaguzi wa Oktoba 2015, pia walikuwa wakizungumzia
majimbo 26 mapya, vipi watagawana, huku kukiwa na mwezi mmoja tu kuanza
kampeni,huku kukiwa na majimbo mapya ambayo hata hayaonyeshi mipaka
ilipo,hivyo ili wakae na wataalam ili wajue nini cha kufanya,hii
inaonyesha ni jinsi gani serikali isovyojali wananchi wake, kwa nchi
masikini kama Tanzania kuongeza majimbo ni kujiongezea gharama tu.

No comments:
Post a Comment