Azam
FC ilipumzika jana Jumatatu ili kuondoa uchovu wa kambi ya Zanzibar, ambayo
ilikuwa ni sehemu ya muendelezo wa maandalizi ya msimu ujao unaotarajia kuanza
Agosti 17, mwaka huu kwa kucheza mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya Yanga.
Mabingwa
hao katika programu ya wiki hii wataendelea kucheza mechi za kirafiki, ambapo
kesho Jumatano saa 10.00 jioni itacheza na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Azam
Complex.
Mbali
na mchezo huo, Jumamosi ijayo itakipiga na Ruvu Shooting nyumbani kwao kwenye
Uwanja wa Mabatini, Pwani, mechi ambayo itafunga maandalizi ya Azam FC wiki hii
kabla ya kupumzika Jumapili ijayo.
Mpaka
sasa Azam FC imeshacheza mechi tano za kirafiki zote ikishinda kwa kuzilaza,
Friends Rangers (2-1), Ashanti United (1-0), Mshikamano (1-0), Wilaya ya Mjini
(1-0) na Taifa ya Jang’ombe (1-0).
Kikosi
hicho kinakaribia kufikisha mwezi sasa tokea kilipoanza kufundishwa na makocha
wapya kutoka Hispania, Kocha Mkuu Zeben Hernandez, Msaidizi wake, Yeray Romero,
Kocha Mkuu wa Viungo, Jonas Garcia, Msaidizi wake, Pablo Borges, Kocha wa
Makipa, Jose Garcia na Mtaalamu wa Viungo, Sergio Perez Soto.
No comments:
Post a Comment