Hati za
Makubaliano hayo zimetiwa saini Jijini Dar es salaam, kati ya Mkurugenzi wa
Shirika la USAID, Bi. Sharon Cromer, na Katibu Mkuu waWizara ya Fedha na
Mipango Dkt. Servacius Likwelile.
Msaada huo ni sehemu ya dola Milioni 800, sawa na zaidi ya shilingi Trilion1.76 ambazo serikali ya Marekani kupitia USAID, imepanga kuipatia Tanzania ili kufanikisha Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa katika kipindi cha miaka mitano ijayo, wenye lengo la kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo mwaka 2025.
Kiasi hicho cha fedha kitatumika na serikali ya Tanzania kupitia mfuko mkuu moja kwa moja wakati kiasi kingine kitatumiwa na Taasisi zisizokuwa za kiserikali zinazofanya shughuli zake hapa nchini kufanikisha malengo ya msaada huo.
Miradi iliyopewa kipaumbele ni pamoja na kupambana na UKIMWI na Kifua Kikuu, Uzazi wa Mpango, Kupunguza vifo vya mama na mtoto, kukuza utawala wa kidemokrasia, Usimamizi wa Rasilimali za Taifa, na kuwekeza kwenye sekta ya umeme ili kuimarisha sekta ya viwanda na uzalishaji mali.

CHANZO ISSA MICHUZI
No comments:
Post a Comment