NAIBU Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Annastazia Wambura amewataka washiriki wanaoenda
kuwakilisha nchi kwenye mashindano ya Olimpiki mwaka huu Rio De Jeneiro nchini
Brazil kujituma na kuhakikisha wanafanya vizuri ili kurudi na medali.
Wambura
ameyasema hayo leo wakati wa kukabidhi bendera kwa timu za kuogelea, judo na
riadha katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.
Akiwa anawakabidhi bendera hiyo, Wambura amewaasa wanamichezo hao kutumia fursa nyingine ya kujifunza zaidi kwani kama wataenda kukutana na mataifa mengine mbalimbali.
Wambura amesema kuwa wanapokwenda kuiwakilisha waamini kuwa macho na masikio ya watanzania wote yapo kwao kwahiyo wajitahidi kadri ya uwezo wao kuweza kuhakikisha watakapokuwa wanarejea basi waje wakiwa wamevaa medali zao.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania , Filbert Bayi amesema kuwa kwa mwaka huu washiriki wamekaa kambi katika sehemu tofauti nchini na wengine wakiwa nje ya nchi na hilo.limefanikisha kuweza kujifua vyema ili kuweza kurejesha ushindi nyumbani. Hilal ameweza kuweka kambi nchini Dubai, Magdalena alikuwa nchini Australia. Andrew aliweka kambi chuo cha polisi Moshi na wanariadha waliweka kambi mkoa wa Arusha.
Washiriki kwa upande wa riadha ni Alphonce Simbu, Said Makula l, Fabian Naasi na Sarah Makela. Timu ya kuogelea inawakilishwa na Hilal Hilal na Magdalena Moshi na Judo ni Andrew Mlungu. Huku timu ya kwanza ikitarajiwa kuondoka alfajiri ya leo wakiambatana na daktari wa timu Nasoro Matuzya.

No comments:
Post a Comment