Je kweli Simba watahitaji kutumia mbinu na akili kushinda katika mchezo wa kesho?Tusubiri tuone……
Pazia la Ligi Kuu Bara msimu mpya wa
2016/2017 litafunguliwa kesho Jumamosi
Agosti 20, timu 14 zitakuwa katika viwanja tofauti kusaka ushindi katika
mechi zao za kwanza za msimu, mechi zote zitakuwa na ushindani mkubwa kwani
kila timu haitaki kubaki nyuma, kila mmoja anahitaji kuanza kwa ushindi.
Simba
vs Ndanda
Licha ya maandalizi mazuri
waliyokuwa nayo Simba haitakuwa rahisi kwao kupata ushindi dhidi ya Ndanda kama
wanavyodhani, Wekundu wa Msimbazi wanatarajiwa kupata upinzani mkubwa siku
hiyo kutoka kwa Ndanda, timu hiyo kutoka Mtwara ni moja ya klabu ngumu Ligi Kuu
na wanacheza kwa ushirikiano na kujituma muda wote dimbani, kwa
hakika patachimbika.
Simba inataka kurejesha heshima
yake, na Ndanda wanataka kudhihirisha kuwa si wa kudharauliwa.
Mtibwa
vs Ruvu Shooting
Achana na vita vya uwanjani, vita
kubwa ipo baina ya wasemaji wa klabu hizo, ambao ni marafiki wakubwa, Mtibwa
Sugar ambayo msemaji wake ni Thobias Kifaru na Ruvu Shooting ambayo
inawakilishwa na Masau Bwire, wasemaji hawa ndio wanafanya mechi hii kuwa na
mvuto hasa kutokana na maneno yao ya kejeli nje ya uwanja.Msimu uliopita Kifaru
alimmisi sana swahiba wake masau na sasa vita vinaendelea.
Stand
utd v/s mbao fc
Timu ya mbao inaingia uwanjani
ikiwa imependa ligi kuu msimu huu huku
ikicheza na timu ambayo imekubwa sana na migogoro ya kiuongozi huku kila timu
inahitaji kushinda katika mchezo wa kesho
lakini wengi wakiipa nafasi timu ya stand utd kutokana na uzoefu wa ligi hiyo.
Majimaji
v/s tanzani prisons
Huu ni mchezo mwngine pia
tukiushuhuda kesho pale maji maji
watakapowakaribisha Tanzania prisons
huku timu zote zikiwa na uzoefu na mikiki mikiki ya ligi kuu Tanzania bara.
Azam
fc v/s African Lyon
Mchezo huu utachezwa usiku pale
chamanzi badala ya saa kumi jioni
kutokana na kesho jumaosi kutakuwa na mazoezi ya timu ya afrika kusini chini ya
umri wa miaka 17 kuutumia uwanja wa chamanzi kwa ajili ya kufanya mazoezi.
HATA
HIVYO
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaonya timu kuchezesha wachezaji wa kigeni
kama hawana vibali vya kuishi, kufanya kazi na leseni inayomruhusu kucheza ligi
husika kwa mujibu wa sheria za nchi na kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara.
Vibali
vya kuishi na kufanya kazi vinatolewa na Idara ya Uhamiaji Tanzania (Uhamiaji)
wakati leseni ya kucheza inatolewa na TFF. Vilevile tumeziagiza klabu kulipia
ada za ushiriki kwa kila timu; leseni za wachezaji, ada za wachezaji na ada za
mikataba. Mchezaji hatapewa leseni ya kucheza kama uongozi wa timu
hautakamilisha taratibu za malipo.
TFF
linapenda kuzikumbusha timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
kwamba hatutatoa leseni ya mchezaji yeyote ambaye timu haikuleta mkataba wakati
wa maombi ya usajili, hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 68 vipengele vya 1, 2, 3
na 8 ya Ligi Kuu ya Tanzania toleo la 2016/2017.
Kila
timu inatakiwa kuleta nakala tatu za mkataba wa mchezaji, ili kamati ya katiba,
sheria na hadhi za wachezaji iweze kupitia na TFF iweze kuidhinisha mikataba
hiyo. Baada ya hapo timu na mchezaji, watakuja kuchukulia mikataba hiyo hapa
TFF.